TAMAA TAMU
Ni kweli tendo la ndoa ni tamu kivyakevyake na huwezi kulinganisha
na kitu kingine chochote lakini tunapaswa kuangalia jinsi tamaa ya utamu huo
ilivyo na jinsi ya kuitumia kujenga penzi linalotosheleza. Asilimia kubwa ya
wanaume wanaonekana kama vile hawawezi kutosheka kuwa na mwanamke mmoja na pia
wapo baadhi ya wanawake ambao nao wanaona kuwa hawawezi kutosheka na mwanaume
mmoja.
Wataalamu wa sayansi ya mapenzi wamegundua kuwa kila mtu anahitaji
mambo fulani ili aweze kujisikia kuwa ametosheka na tendo la ndoa na hali hiyo
inaitwa kwa kiingereza FETISH. FETISH ni jambo ambalo unaliona kuwa bila ya
kuwepo kwa jambo hilo huwezi kutosheka na tendo la ndoa na kwa bahati mbaya
watu wengi hawajui kuwa wanao udhaifu wa aina hii,udhaifu wa ajabu sana.
Neno FETISH limetokana na lugha ya Kireno FETICO,neno hilo
hutumika ikimaanisha nguvu ya kichawi. Kila mmoja anao udhaifu wa aina
hii japo hatufahamu jinsi nguvu yake inavyotuendesha katika mahusiano yetu ya
kimapenzi. Hali ya mtu kupenda mwanamke mwenye hipsi na makalio ya aina fulani
hiyo iko katika kundi la fethish, mwanamke kupenda mwanaume mrefu mwenye
misuli ,mwanaume mwenye sauti nzito na hiyo ni fetishi yake.Mwanamke
anayependelea mwanaume mwenue kifua kilicojaanywele kwa mfano atapata shida
kuridhika iwapo mumewe hana nywele hizo.Mfano huo unaweza kuupeleka kwa ukubwa
wa uume pia.
Kuna aina nyingi za MAFETISHI na nyingine ni za ajabu sana lakini
ambazo zimetawala kwa watu wengi ni hizi zifuatazo:-
(1) VOYEURISM
Hii ni tamaa inayojitokeza pale uonapo maumbile ya mwili wa mtu wa
tofauti na jinsia yako. Tamaa hii inachochewa na nguvu na uvaaji wa nguo
zinazobana au zinazoacha wazi maeneo fulani ya mwili.
(2) PYGOPHILIA
Hii ni tamaa ya kutamani mtu mwenye makalio ya muundo fulani au
kujikuta unapata msisimko mkali uonapo mtu mwenye makalio ya aina hiyo tamaa
hii inawasumbua zaidi wanaume ambao wanataka wanawake wote wawe na makalio kama
ya Jenifer Lopez (JLO).Utafiti uliofanyika na mashirika ya bima huko uingereza
umeonyesha kuwa wanaume wengi husababisha ajali za magari hasa wakati wa
kiangazi ambapo wanawake wengi huvaa nguo fupi na zenye kubana na kuonyesha
uzuri wa makalio.
(3) RETIFISM
Hii ni tamaa inayoamshwa pale uonapo mwanamke aliyevaa viatu virefu
(mchuchumio).
(4) TRICHOPHILIA
Hii ni tamaa ambayo hujitokeza kwa mtu akutanapo na mtu mwenye
aina fulani ya nywele au wigi fulani la nywele. Hii inaweza kuwa hata nywele za
kifuani.
(5) DOMINATION AND
SUBMISSION
Hii tamaa imewabana watu wengi na hawajui kuwa
inawatawala na hivyo kushindwa kujua jinsi ya kukabiliana nayo ili kuongezea
penzi kati yao. Mara nyingi wakati wa tendo la ndoa mwanaume huwa juu na
mwanamke huwa chini na wengi huona kuwa ni hali ya kawaida kabisa lakini kwa
kutokujua nguvu ya desturi hiyo wengi wamewazoesha wapenzi wao.Mindo huo
utumikapo mara kwa mara unamfanya mwanaume ajione zaidi kuwa yeye ndiye mbabe
na hahitaji ushauriau msaada toka kwa mkewe. Kwa mpenzi ambaye yeye anapata
raha zaidi kwa kumfanyia mambo fulani fulani mpenzi wake ni muhimu apewe nafasi
hiyo ili ajione kuwa ni wa muhimu na mwenye nguvu. Hivyo basi iwapo
mpenzi wako atakuwa mwenye haraka au asiependelea tendo la ndoa lichukue zaidi
ya nusu saa huyo atakuwa anajiharibia uhusiano wake mwenyewe bila kujua. Watu
wengi huchanganyikiwa hapa kwani kuna wengine ambao wanapenda kutoa starehe kwa
wapenzi wao wakiwa wametulia jambo ambalo humfanya mpenzi aboreke.
Wengine hupendelea kubadilishana nafasi kwa kupokezana mmoja amwandae
mwenziwe na baadae na wao wanataka watulie na kumwachia mpenzi kazi ya kumletea
utamu wa tendo la ndoa DOMINATION NA SUBMISSION kwa Kiswahili ni KUTAWALA
NA KUTAWALIWA (au kwa maneno mengine ni kama kukandamiza na kukandamizwa). Ni
muhimu kwa wapendanao kutambua umuhimu wa mtindo huu kwani una nguvu kubwa sana
ukitumiwa vizuri katika kipindi cha tendo la ndoa. Katika utafiti wangu juu ya
kuongezea utamu wa tendo la ndoa nilifikia hatua ya kuanza kuangalia jinsi
wasagaji, yaani wanawake wanaofanya mapenzi na wanawake wenzao na huko niliona
nguvu ya mtindo huo. Baada ya kuangalia kwa muda fulani nilielewa kwanini
mwanamke ambaye ameingia kwenye usagaji atapata shida kubwa kufurahia tendo la
ndoa na mwanaume na wengi hufikia hatua ya kuwachukia wanaume.
Changamoto kwa wapendanao ni kwamba upo umuhimu wa kutumia mtindo
huu wa KUTAWALA NA KUTAWALIWA katika kuboresha utamu wa tendo la ndoa na
kuondosha hali ya mpenzi kuboreka na mpenzi wake wa muda mrefu. Ili uweze
kufanikiwa katika hili ni muhimu upige vita woga na aibu. Nakutakia heri katika
kutengeneza utamu zaidi wa tamaa ya tendo la ndoa.
Ni mafunzo kamili kwa pande zote mbili!
ReplyDelete