Monday, November 18, 2013

KANUNI MUHIMU KWA WANAWAKE

KANUNI MUHIMU KWA WANAWAKE

(1)        Kuwa mwanamke ambaye anahitajiwa na mwanaume na sio mwanamke anayehitaji mwanaume.

Tafsiri yake
Kibaologia ubongo wa mwanaume una tofauti kubwa ukilinganisha na wa mwanamke na hivyo utendaji wao na mahitaji yao yana utofauti pia. Uwezo wa kuzungumza wa mwanamke ni mkubwa kuliko wa mwanaume, yaani kwa siku moja mwanamke ana uwezo wa kuongea maneno 20,000 wakati mwanaume ana uwezo wa kuongea maneno 7,000 kwa siku. Mwanamke asipojua njia za kuoanisha tofauti hizi atamchukiza mwanaume bila ya yeye kujua na ndio maana Biblia inasema “kila mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake. Bali aliyempumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe (Mithali 14:1).Ili uweze kuwa mwanamke ambaye mwanaume anamhitaji inakupasa usome mahitaji ya mwanaume vizuri ili uweze kuyatimiza kikamilifu na kumtosheleza kabisa.

(2)        Mwanaume akikuacha au kukudharau ni hasara yake na sio yako.

Tafsiri yake
Iwapo una uhakika wa kuifuata vizuri kanuni ya kwanza na kwa bahati mbaya ukapata mwanaume asieuona uthamani wako usibabaike kabisa. Yeye ndie kipofu haoni thamani yako na kuandoka kwake toka katika maisha yako maana yake Mungu anakuelekeza kwa mwanaume mwingine aliye bora kuliko huyo. Biblia inakuagiza “Tulia ujue ya kuwa mimi ni Mungu nitatukuzwa katika mataifa” Zaburi 46:10.

(3)        Onekana kama kipepeo lakini ng’ata kama nyuki.

Tafsiri yake
Biblia inasema kwamba wanawake wanapaswa wajipambe kwa utu wa moyoni usioonekana yaani roho ya upole na utulivu na hekima (Petro 3:4). Mwanamke pamoja na mapambo yote na uzuri wa nje ni muhimu tabia yake ionyeshe utulivu na upole. Kipepeo haumizi mtu na anapendeza kwa muonekano wake lakini hivyo peke yake haitoshi kuvuta na kutunza penzi la mwanaume. Hivyo basi ni muhimu mwanamke mara nyingine awe kama nyuki, yaani aonyeshe ukali pale anapoonelewa. Ajenge uwezo wa kuelezea hisia zake bila ya uoga wowote ule.KUMBUKA kuwa wanaume hupenda wanawake wanaoleta changamoto zinazojenga na sio wenye unafiki.
Kwa kufanya hivyo ataweza kudumisha penzi katika msingi wa haki na ukweli na sio unafiki. Fuata maneno ya BWANA YESU “kuweni na busara kama nyoka  na wapole kama njiwa (Mt 10:16).

(4)        Usianzishe ugomvi bali zifahamu njia za kumaliza ugomvi

Tafsiri
Ukiwa mpole utapenda sana kutafuta kumwelewa mwenzio badala ya kumhukumu ,ukimhukumu hasira huja haraka na hivyo kuanzisha ugomvi. Epuka kukurupuka na kusema maneno harakaharaka .Jifunze kutulia japo umeumia au kukasirika. Kwa kufanya hivyo utaweza kuona kwa urahisi njia za kujibu na kutatua migogoro katika mahusiano yako.  

(5)        Kuwa mpenzi na sio mpiganaji lakini siku zote pigania unachokipenda

Tafsiri
Unapoamua kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu jitahidi kumpa mapenzi yote kwa moyo wote. Pamoja na hayo yote yatokeapo magumu kuwa mstaarabu kuepuka hali ya ugomvi kwa kujizuia kupaza sauti au kuongea maneno makali. Jambo la msingi tambua mambo muhimu na usikubali mpenzi wako ayapuuzie mambo hayo kwa urahisi. Jenga hoja nzito za kupigania haki yako ya kuishi maisha ya furaha na amani.

(6)        Kupata kitu ambacho hujawahi kukipata ni lazima ufanye vitu ambavyo hujawahi kufanya.

Tafsiri
Ni rahisi sana kufanya vitu ulivyozoea na kufurahia hali hiyo mpaka pale itakapotokea shida fulani  inayohusiana na kitu ulichokizoea .Ili uweze kuendelea kufurahia uhusiano wako zaidi ni muhimu utafute vitu vipya vya kupamba na kuimarisha uhusiano wako. Hapa inahitaji ubunifu, uchunguzi na ujasiri wa kujaribu jambo ambalo hujawahi kukutana nalo. Kwa kuwa kila siku tunakutana na mambo mengi upo uwezekano mkubwa wa mtu kubadili mtazamo wake juu yako na ukapata matatizo katika uhusiano wako. Kuleta vitu vipya huleta msisimko mkubwa na iwapo wewe ndio utakuwa chanzo cha msisimko huo basi utathaminiwa na kupendwa zaidi.

(7)        Kabla hujauliza kwanini fulani hakupendi, jiulize kwanini unajali sana juu ya hilo

Tafsiri
Kumpenda mtu mwingine ni kitu rahisi sana na sisi wote tumo katika kundi hilo lakini kumfanya mtu mwingine akupende  au aendelee kukupenda sio rahisi kabisa.Pale unapotamani mtu fulani akupende kwanza jiangalie mwenyewe vizuri je kama mtu huyo anapenda mtu mwenye maumbile mazuri unayo sifa hiyo?. Kama anapenda mtu mfupi wewe unayo sifa hiyo? Na kama anataka mtu mwenye elimu au mwenye pesa wewe umo kwenye kundi hilo.? Hayo yanaweza kuwa maswali magumu kwa wengi lakini swali lingine rahisi kwa kila mtu ni je ni kwa vipi mimi nitaweza kuchangia furaha yake zaidi ya mtu mwingine yoyote?. Ukiweza kujibu swali hili unanafasi kubwa ya kujisogeza kwake na yeye akakuona kuwa kweli unafaa, lakini ukijisogeza bila kuwa na sifa za kutosha unatafuta maumivu ya moyo. Madhaifu kama aibu, hasira, woga, unene kupita kiasi, uvivu au kupenda kuongea bila ya kuchoka yanaweza kuharibu penzi hata kama utapata mtu mwenye penzi la kweli. Jichunguze kama vile Biblia isemavyo.“ Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na angalia asianguke (1Wakorintho 10:12)

“Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani, jithibitisheni wenyewe (2 Wakorintho 13:5).  

BOYFREND KANITUPA BILA HURUMA

BOYFREND KANITUPA BILA HURUMA

Doctor, mimi ni binti mwenye umri wa miaka 24 na nimekuwa na uhusiano na kaka mwenye umri wa miaka 27U. Uhusiano wetu hadi leo ulikuwa na umri wa miaka 2. Kwa kweli nilimpenda sana Alex kutokana na tabia zake na muonekano wake pia.

Kutokana na mambo aliyokuwa ananifanyia na kuniambia niliamini kabisa kuwa yeye ndiye mume ambaye Mungu alinipangia .Nilishangaa wiki iliyopita alivyoanza kubadilika na nilipomuuliza alisema “Hisia zangu juu yako zimebadilika na sijui ni kwanini” niliumia sana kusikia hilo na siku mbili baadae aliniambia wazi kuwa hatuwezi kuendelea kuwa wapenzi tena. Doctor, inakuwaje mtu kuweza kubadilika haraka sana kiasi hicho? Naumia sana hadi nashindwa kulala na kula chakula na najikuta nalia mara kwa mara na nashindwa kufanya kazi. Leo nimeangalia kwenye facebook nimegundua kuwa sasa ana msichana mwingine. Doctor nifanyeje?.

JIBU:  Pole sana dada yangu na napenda kukuambia kuwa hauko peke yako katika mtego uliokunasa na kukujeruhi ukweli ni kwamba mchakato wa wewe kuachwa ulianza muda mrefu na kwa bahati mbaya hukuwa na utaalamu wa kuona dalili zake.

Naamini kuwa nia yako ya kuniandikia barua pepe ni kutafuta njia ya kuweza kumrudisha aendelee kuwa mpenzi wako kwani tayari umegundua kupitia facebook kuwa amepata  mwanamke mwingine.

Kabla sijakupa njia ya kupita kumrudisha mpenzi wako ni muhimu uangalie kwa makini sababu kuu za wewe kutetea arudi je ni kweli kwa maneno, matendo na mwenendo wake alikuletea furaha na hali ya kujivunia kutokana na sifa alizonazo? Labda alikuwa ni mwenye hasira au alikuwa na wivu mchafu, au alikusaliti na kutembea na mtu mwingine au alikuwa sio mkweli mara kwa mara au alikuwa hajali hisia zako na maoni yako?. Au jiulize swali linguine gumu, je unao uhakika kuwa ulikuwa unampa sababu za kutosha kabisa kufurahia maisha yake kutokana na wewe kuwa katika maisha yake?.




(1)        Angalia makosa
Kuachana kwa wapenzi huwa hakutokei bila sababu yoyote na hivyo iwapo unataka mpenzi wako akurudie ni muhimu sana kwanza uangalie kosa linalowatenganisha ni nini.Angalia ni jinsi gani mwenzio anaoliona kosa kama ni la kwako,upo uwezekano kuwa amelikuza zana na ikamfanya asiyaone mazuri yako yote.Kama kosa ni lake je angalini jinsi gani umelipokea najinsi gani limekuumiza na mwisho angalia je hukumu ulioitoa na kumwambia katika maongezi yenu ya mwisho ni sahihi au je ulitoa hukumu kubwa zaidi ya kosa lenyewe?

(2)        Kwepa wanaume au wanawake
Iwapo mtu uliempenda amekuacha na hujui kwamba huenda akatamani mrudiane ni muhimu sana kwako ukwepe kujenga ukaribu na watu wa jinsia tofauti na wewe ili kumfanya mwenzio aendelee kuona kuwa nafasi yake bado ipo wazi. Kujaribu kujihusisha na watu wa jinsia tofauti na yako kwa nia ya kumtia wivu ni sawa na kumfukuza kabisa mtu huyo.HIVYO epuka ukaribu wowote na wanaume au wanawake katika kipindi chote cha kuokoa uhusiano wenu.

Ili kuweza kumrudisha na aweze kukung’ang’ania fuata hatua zifuatazo:-
(1)        Usimpe faida ya yeye kuona kuwa amefanikiwa kukuumiza na kukutoa machozi. Jifanye kama vile hukuumia kabisa. Akiona kuwa hajafanikiwa kukuumiza ataanza kujiuliza maswali mengi na moja kati ya jibu atakalolipata ni kuangalia hasara aliyoipata kutokana na wewe kutokuwepo maishani mwake (hii itafanya kazi vizuri kama una uhakika kuwa ulikuwa na mchango mkubwa katika kumletea furaha katika mazungumzo na mwenendo wako, ufundi wako katika tendo la ndoa na usafi kwa ujumla).

(2)        Endelea kumpigia simu na kwa uchangamfu mkubwa mweleze matukio mbalimbali yanayoendelea katika maisha yako. Kwa kufanya hivi ataona kwa hakika jinsi gani ulivyo na nguvu katika nafsi yako ya kupambana na kufanikiwa katika maisha. Jambo  LA KUONYESHA KUWA UNAWEZA KUANGUKA NA KUINUKA NA KUENDELEA NA MAISHA YAKO  ni jambo ambalo huwavuta wanaume japo hawatakuambia. Jitahidi kujizuia usimpigie simu kila siku, panga siku mbili katika wiki ambapo utampigia simu kwa mtindo ulioeleza hapo juu, yaani uchangamfu uwe kiungo kikubwa. Tafadhali kabla hujampigia mtumie SMS isamayo, “samahani naweza kukupigia sasa?” kwa kufanya hivyo utamwonyesha kuwa unaheshimu uhuru wake na usingependa mpenzi wake mpya aanzishe ugomvi kwa sababu yako wewe.

(3)        Kwa kufanya mambo hayo mawili utakuwa umesababisha maswali mengi nafsini mwake na yeye mwenyewe ataanza kukuchokoza kwa SMS au kwa kukupigia simu. Aanzapo hilo hapo jitahidi kujibu SMS zake katika hali ionyeshayo uchangamfu na pia akupigiapo simu jitahidi kuwa mchangamfu vya kutosha. Katika mazungumzo yenu kwa SMS au kwa simu jitahidi kutaja  jina lake mara kwa mara kwa kufanya hivyo unajiunganisha upya katika nafsi yake hali ambayo itaendelea kumsumbua moyoni mwake.

(4)        Hatua hizo zitamfanya apate hamu ya kukuona na pale mtakapopanga kuonana hakikisha kuwa uchangamfu wako unaambatana na tabasamu lenye nguvu ya kuyeyusha barafu iliomo moyoni mwake. Kumbuka tabasamu lako ndilo ambalo lina nguvu ya kumkumbusha mema yote aliyopata toka kwako na utamu wa penzi lako.Nguvu ya uchangamfu wako na mazungumzo yako yataanza kumsumbua pale atakapoachana nawe kwenda kwake. Wakati unapokuwa nae jitahidi kumshikashika kwa mkono aidha mapajani au eneo toka kwenye bega hadi kiwiko cha mkono. Sayansi inathibitisha kuwa njia hii inasababisha mtu kukuthamini zaidi na atapata shida kusahau mazuri yako na hivyo kutafuta njia ya kuunganishwa nawe kwa  upya.

ANGALIZO
 Ni muhimu uzingatie kuwa japokuwa mmetengana huenda bado anakupenda na kwamba huenda kuna jambo ambalo limemchanganya na kwa kipindi hicho akakuona kuwa hufai lakini baadae atazinduka na kutaka kukurudia. Aonapo kuwa bado mlango uko wazi atakuwa mwepesi kurudi. Umuhimu wa jambo hili utauona vizuri iwapo kuachana kwenu kulitokea katika hali ya ghafla au baada ya kutupiana maneno makali

Ni muhimu ujichunguze iwapo kabla hamjatengana hukuwa na wivu wa kupita kiasi, ulishindwa kutimiza ahadi zako mara kadhaa, angalia kama kuna mambo ambayo ulimkatalia bila sababu ya kimsingi, tathmini iwapo una ufundi wa kutosha kumfanya mwanaume afurahie tendo la ndoa kikamilifu na hasa uwezo wa kumsaidia mwanaume aweze kusimamisha uume wake mara nyingine na nyingine na zaidi ya hayo. Kwa kuwa tendo la ndoa ni chakula muhimu sana kwa mwanaume aliyekamilika iwapo atakuhitaji katika eneo hilo basi hakikisha kuwa huwi mvivu na una nyenzo za kutosha kumpagawisha.

Monday, October 21, 2013

KUKATALIWA KATIKA MAPENZI



 MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOKATALIWA
(1)        Mwenzio anayo haki ya kutumia uhuru wake wa kuchagua anachokipenda na kuacha asichokipenda.

(2)        Mwenzio anathamini hisia zake kuliko zako.

(3)        Labda kwa sasa hayupo tayari jaribu baadaye.

(4)        Iwapo unakataliwa na watu wengi jichunguze mwenyewe. Huenda huna tabia nzuri au mvuto wako mdogo sana.

Toa maoni yako. Pia soma ukurasa wa HABARI MPYA kupata mwendelezo wa mada hii...

UKWELI JUU YA UKUBWA WA UUME



Yafuatayo ni majumuisho ya matokeo ya tafiti mbalimbali juu ya ukweli juu ya ukubwa wa uume. Tafiti hizo zimefanywa na wanasayansi wa mapenzi toka nchi za Ujerumani, Uingereza, Sweden, Nigeria na Afrika ya kusini. Jisomee na uone mambo yalivyo matamu usifuate maneno ya mitaani na jichunguze uone kama uko katika kiwango au la.

(1)        Iwapo wewe ni mwanamke na hupendelei uume mkubwa basi wewe ni wa ajabu.

(2)        Wanawake wengi hupendelea uume mkubwa zaidi ya wanaume kupendelea matiti au makalio makubwa.

(3)        Kwa wastani wanaume wengi wana uume wenye urefu wa kati ya nchi 6 (CM 15) na nchi 7 (CM18) na unene kati ya nchi 5 (CM12) na nchi 51/2 (CM 131/2).

...endelea ukurasa wa HABARI MPYA..Bofya hapa...UKWELI KUHUSU UKUBWA WA UUME

Pia USIKOSE KUTEMBELEA BLOG HII wiki lijalo kutakuwa na mambo mengi mapya.