BOYFREND
KANITUPA BILA HURUMA
Doctor,
mimi ni binti mwenye umri wa miaka 24 na nimekuwa na uhusiano na kaka mwenye
umri wa miaka 27U. Uhusiano wetu hadi leo ulikuwa na umri wa miaka 2. Kwa kweli
nilimpenda sana Alex kutokana na tabia zake na muonekano wake pia.
Kutokana
na mambo aliyokuwa ananifanyia na kuniambia niliamini kabisa kuwa yeye ndiye
mume ambaye Mungu alinipangia .Nilishangaa wiki iliyopita alivyoanza kubadilika
na nilipomuuliza alisema “Hisia zangu juu yako zimebadilika na sijui ni
kwanini” niliumia sana kusikia hilo na siku mbili baadae aliniambia wazi kuwa
hatuwezi kuendelea kuwa wapenzi tena. Doctor, inakuwaje mtu kuweza kubadilika
haraka sana kiasi hicho? Naumia sana hadi nashindwa kulala na kula chakula na
najikuta nalia mara kwa mara na nashindwa kufanya kazi. Leo nimeangalia kwenye
facebook nimegundua kuwa sasa ana msichana mwingine. Doctor nifanyeje?.
JIBU: Pole sana dada yangu na napenda kukuambia kuwa
hauko peke yako katika mtego uliokunasa na kukujeruhi ukweli ni kwamba mchakato
wa wewe kuachwa ulianza muda mrefu na kwa bahati mbaya hukuwa na utaalamu wa
kuona dalili zake.
Naamini
kuwa nia yako ya kuniandikia barua pepe ni kutafuta njia ya kuweza kumrudisha
aendelee kuwa mpenzi wako kwani tayari umegundua kupitia facebook kuwa amepata mwanamke mwingine.
Kabla
sijakupa njia ya kupita kumrudisha mpenzi wako ni muhimu uangalie kwa makini
sababu kuu za wewe kutetea arudi je ni kweli kwa maneno, matendo na mwenendo
wake alikuletea furaha na hali ya kujivunia kutokana na sifa alizonazo? Labda
alikuwa ni mwenye hasira au alikuwa na wivu mchafu, au alikusaliti na kutembea
na mtu mwingine au alikuwa sio mkweli mara kwa mara au alikuwa hajali hisia
zako na maoni yako?. Au jiulize swali linguine gumu, je unao uhakika kuwa
ulikuwa unampa sababu za kutosha kabisa kufurahia maisha yake kutokana na wewe
kuwa katika maisha yake?.
(1)
Angalia
makosa
Kuachana kwa wapenzi huwa hakutokei bila sababu yoyote
na hivyo iwapo unataka mpenzi wako akurudie ni muhimu sana kwanza uangalie kosa
linalowatenganisha ni nini.Angalia ni jinsi gani mwenzio anaoliona kosa kama ni
la kwako,upo uwezekano kuwa amelikuza zana na ikamfanya asiyaone mazuri yako
yote.Kama kosa ni lake je angalini jinsi gani umelipokea najinsi gani
limekuumiza na mwisho angalia je hukumu ulioitoa na kumwambia katika maongezi
yenu ya mwisho ni sahihi au je ulitoa hukumu kubwa zaidi ya kosa lenyewe?
(2)
Kwepa
wanaume au wanawake
Iwapo mtu uliempenda amekuacha na hujui kwamba huenda
akatamani mrudiane ni muhimu sana kwako ukwepe kujenga ukaribu na watu wa
jinsia tofauti na wewe ili kumfanya mwenzio aendelee kuona kuwa nafasi yake
bado ipo wazi. Kujaribu kujihusisha na watu wa jinsia tofauti na yako kwa nia
ya kumtia wivu ni sawa na kumfukuza kabisa mtu huyo.HIVYO epuka ukaribu wowote
na wanaume au wanawake katika kipindi chote cha kuokoa uhusiano wenu.
Ili
kuweza kumrudisha na aweze kukung’ang’ania fuata hatua zifuatazo:-
(1)
Usimpe faida ya yeye kuona kuwa amefanikiwa
kukuumiza na kukutoa machozi. Jifanye kama vile hukuumia kabisa. Akiona kuwa
hajafanikiwa kukuumiza ataanza kujiuliza maswali mengi na moja kati ya jibu
atakalolipata ni kuangalia hasara aliyoipata kutokana na wewe kutokuwepo
maishani mwake (hii itafanya kazi vizuri kama una uhakika kuwa ulikuwa na
mchango mkubwa katika kumletea furaha katika mazungumzo na mwenendo wako,
ufundi wako katika tendo la ndoa na usafi kwa ujumla).
(2)
Endelea kumpigia simu na kwa uchangamfu
mkubwa mweleze matukio mbalimbali yanayoendelea katika maisha yako. Kwa kufanya
hivi ataona kwa hakika jinsi gani ulivyo na nguvu katika nafsi yako ya
kupambana na kufanikiwa katika maisha. Jambo LA KUONYESHA KUWA UNAWEZA KUANGUKA NA KUINUKA
NA KUENDELEA NA MAISHA YAKO ni jambo ambalo
huwavuta wanaume japo hawatakuambia. Jitahidi kujizuia usimpigie simu kila
siku, panga siku mbili katika wiki ambapo utampigia simu kwa mtindo ulioeleza
hapo juu, yaani uchangamfu uwe kiungo kikubwa. Tafadhali kabla hujampigia
mtumie SMS isamayo, “samahani naweza kukupigia sasa?” kwa kufanya hivyo
utamwonyesha kuwa unaheshimu uhuru wake na usingependa mpenzi wake mpya
aanzishe ugomvi kwa sababu yako wewe.
(3)
Kwa kufanya mambo hayo mawili utakuwa
umesababisha maswali mengi nafsini mwake na yeye mwenyewe ataanza kukuchokoza
kwa SMS au kwa kukupigia simu. Aanzapo hilo hapo jitahidi kujibu SMS zake
katika hali ionyeshayo uchangamfu na pia akupigiapo simu jitahidi kuwa
mchangamfu vya kutosha. Katika mazungumzo yenu kwa SMS au kwa simu jitahidi
kutaja jina lake mara kwa mara kwa
kufanya hivyo unajiunganisha upya katika nafsi yake hali ambayo itaendelea
kumsumbua moyoni mwake.
(4)
Hatua hizo zitamfanya apate hamu ya kukuona
na pale mtakapopanga kuonana hakikisha kuwa uchangamfu wako unaambatana na
tabasamu lenye nguvu ya kuyeyusha barafu iliomo moyoni mwake. Kumbuka tabasamu
lako ndilo ambalo lina nguvu ya kumkumbusha mema yote aliyopata toka kwako na
utamu wa penzi lako.Nguvu ya uchangamfu wako na mazungumzo yako yataanza
kumsumbua pale atakapoachana nawe kwenda kwake. Wakati unapokuwa nae jitahidi
kumshikashika kwa mkono aidha mapajani au eneo toka kwenye bega hadi kiwiko cha
mkono. Sayansi inathibitisha kuwa njia hii inasababisha mtu kukuthamini zaidi
na atapata shida kusahau mazuri yako na hivyo kutafuta njia ya kuunganishwa
nawe kwa upya.
ANGALIZO
Ni muhimu uzingatie kuwa
japokuwa mmetengana huenda bado anakupenda na kwamba huenda kuna jambo ambalo
limemchanganya na kwa kipindi hicho akakuona kuwa hufai lakini baadae
atazinduka na kutaka kukurudia. Aonapo kuwa bado mlango uko wazi atakuwa
mwepesi kurudi. Umuhimu wa jambo hili utauona vizuri iwapo kuachana kwenu
kulitokea katika hali ya ghafla au baada ya kutupiana maneno makali
Ni
muhimu ujichunguze iwapo kabla hamjatengana hukuwa na wivu wa kupita kiasi,
ulishindwa kutimiza ahadi zako mara kadhaa, angalia kama kuna mambo ambayo
ulimkatalia bila sababu ya kimsingi, tathmini iwapo una ufundi wa kutosha
kumfanya mwanaume afurahie tendo la ndoa kikamilifu na hasa uwezo wa kumsaidia
mwanaume aweze kusimamisha uume wake mara nyingine na nyingine na zaidi ya hayo.
Kwa kuwa tendo la ndoa ni chakula muhimu sana kwa mwanaume aliyekamilika iwapo
atakuhitaji katika eneo hilo basi hakikisha kuwa huwi mvivu na una nyenzo za
kutosha kumpagawisha.
No comments:
Post a Comment