MAMBO
10 YANAYOWACHUKIZA WANAUME.
Wanawake wengi huamini kuwa uzuri wa
maumbile ni jambo la muhimu sana kwa mwanaume jambo ambalo sio la msingi kabisa
katika kujenga penzi linalodumu.Uzuri wa maumbile unaweza kumvuta mwanaume
kuanzisha uhusiano lakini sio kitu ambacho kinaweza kuwa nguzo muhimu ya
kudumisha uhusiano huo. Mwanaume anahitaji mwanamke ambae atakuwa chemchemu ya
kudumu ya furaha katika maisha yake. Yafuatayo ni mambo kumi ambayo hunyausha penzi la mwanaume.
1.
Kumpigia simu au kumtumia ujumbe mfupi
(SMS) mara kwa mara na kulaumu pale ambapo mwanaume hapigi simu mara kwa mara
au kutuma SMS. Siku hizi kuna SMS zilizotungwa ambazo zina maneno mazuri mazuri
ya kimashairi na wanawake wavivu huzitumia hizo kuwatumia wanaume kuonyesha
mapenzi yao, ukweli mara nyingi zinakuwa kero kwa wanaume kwa kuwa hazina
uhalisia unaotoka kwa mtumaji. Wanawake wenye tabia hii hawajui umuhimu wa
kumfanya mwanaume akumiss kwa muda fulani. Iwapo sitaki kukushirikisha
ninavyoweza swali lako litanifanya nijisikie vibaya kwako nachukia kusema uongo
hivyo nitakuchukia na kukuona kuwa unataka kunilazimisha kukueleza kila kitu
kilicho moyoni mwangu.
2.
KUKUBALIANA
NA KILA KITU
Mwanamke
ambaye anaogopa kuachwa, kufokewa na yuko tayari kufanya jambo lolote lile ili
kumfurahisha mwanaume anaboa. Sio hilo tu bali inaumiza kuona kuwa umekuwa
mpokeaji zaidi ya mtoaji na hali hii huzalisha uchungu na dharau ambayo
haimsaidii mwanamke. Upo umuhimu wa mwanamke
kuonyesha kuw nayeye ana mawazo mazuri kwa kukataa kukubaliana na kila kitu
anachosema mwanaume.
3.
KUTAKA
KUJUA MAWAZO YA MWANAUME
Mwanaume
anapokaa kimya sio kwamba amekasirika bali anapanga mambo yake na hataki
kuingiliwa. Wanawake wengi waonapo mwanaume yuko kimya hukimbilia kuuliza
“unawaza nini?” swali hili ni kero mbaya sana kwani unaingilia uhuru wa mtu
mwingine. Tatizo hili linaenda pamoja na mwanamke mwenye tabia ya kutaka kwenda
na mumewe kila mahali. Hali hii sisi wanaume tunachukia sana. Iwapo sitaki
kukushirikisha ninavyowaza moyoni mwangu, swali lako litanifanya nijisikie
vibaya kwani nachukia kusema uongo hivyo nitakuchukia na kukuona kuwa unataka
kunilazimisha kukueleza kila kitu kilicho moyoni mwangu.
4. WASIOJISHUGHULISHA VYA KUTOSHA KITANDANI
Mchezo
siku zote huhusisha pande mbili na katika tendo la ndoa ni hivyo hivyo.
Asilimia 85 ya wanawake ni wavivu katika tendo la ndoa jambo ambalo ni kero kwa
wanaume. Kwa kuwa wanaume wana tatizo la nguvu za kiume na kuwahi kumaliza
mwanamke ambaye hajishughulishi wakati wa tendo la ndoa huzalisha hasira kwa
mwanaume. Mwanaume afanyapo tendo la ndoa kwa ufanisi mzuri hasa akirudia zaidi
ya mara moja anakuwa amepunguza makali ya kichocheo (hormone) cha TESTOSTERONE,
kichocheo hicho kikipungua na hasira hupungua. Kutokana na ukweli huo uvivu wa mwanamke
kitandani mara nyingi humkasirisha mwanaume. Kwa kuwa mwanaume huyo hawezi
kumwambia mwanamke mapungufu hayo hasira hiyo hujitokeza katika maeneo mengine
tofauti kabisa jambo ambalo huwashangaza wanawake wengi.
5. KUTUMIA TENDO LA NDOA KAMA SILAHA
Wanaume
wote hupendelea tendo la ndoa hadi katika Biblia ikaandikwa “MSINYIMANE” (2
KORINTHO 7) wanawake kwa kufahamu udhaifu huu wa wanaume wamewanyima wanaume
unyumba kwa manufaa yao na kutumia tendo la ndoa kama adhabu au njia ya
kulazimisha mabadiliko upande wa
mwanaume.Mtazamo na tabia hii hubomoa nyumba.
6. WACHAFU
Hakuna
mtu ambae anafurahi kuwa karibu na mtu anaetoa harufu mbaya. Wanawake wengine
hujisahau na hawana tabia ya kupiga mswaki wakati wa kulala na inapotokea saa
tisa usiku mwanaume anataka tendo la ndoa harufu mbaya toka mdomoni
inamkasirisha mwanaume japo hatalalamika
au kusema lolote. Mwanamke asipotumia maji kujiosha baada ya haja kubwa
apanuapo miguu harufu ya choo ni chukizo kubwa. Kutojiosha baada ya raundi ya
kwanza ya tendo la ndoa husababisha uume uteleze kupita kiasi na wanaume
wengine huishia kutafsiri kuwa mwanamke huyo ana uke mpana jambo ambalo
linawatuma wanaume kufukuzia mabinti wadogo au kuomba mchezo kinyume na
maumbile. Mara nyingi mwanaume alie naye hatasema juu ya udhaifu huu na
utashangaa tu kuona penzi limeshuka na kuendelea kunyauka.
7. VING’ANG’ANIZI
Wanaume
wengi huchukia wanawake ambao hupenda kuwang’ang’ania kiasi ambacho wanajiona kama
wamekuwa mateka au wafungwa gerezani. Wanawake ving’ang’anizi ni wale ambao
hawajiamini na wanaogopa kuachwa au kusalitiwa kila dakika .Pale ambapo
mwanamke anajaribu kumchunga mwanaume kwa kupiga simu mara kwa mara au kuuliza
maswali yasio na msingi. Maswali kama upo wapi, uko na nani? Ulikuwa unaongea
na nani kwenye simu? N.k ni kero kubwa sana kwa mwanaume. Inakuwa ngumu sana
kumfurahisha mtu ambaye muda wote anajiona yuko katika hatari ya kuibiwa,
anakuwa hana amani pale mwenziwe awapo mbali. Hali hii inawachosha sana wanaume
na kutamani kujificha zaidi na zaidi jambo ambalo linamtesa mwanamke alie
king’ang’anizi.
8. WAKANDAMIZAJI HOJA
Wakandamizaji
wa hoja nI wale ambao hupenda kumkumbusha mpenzi wake jambo ambalo tayari
alishamwambia mara kadhaa na mwenzie hajalifanya bado. Mwanamke hufanya hivi
bila kujua kuwa ni jambo la hatari sana. Hali hii huwa kama sumu pale inapokuwa
ina husu udhaifu au makosa fulani kwa kuwa hakuna anaefurahia kukosolewa mara
kwa mara. Kumuuliza mwanaume mara kwa mara kwanini hakufanya jambo fulani
hutafsiriwa kama dharau na hilo laweza kugeuka kuwa sumu kama sauti ya ukali
inatumika. Kumwambia mwanaume afanye jambo ambalo hayuko tayari kulifanya.Ukandamizaji
wa aina hii unanyausha penz taratibu sana. Kwa mfano kuuliza lini atakutambulisha
kwa wazazi au ndugu zake,lini anapamga mfunge ndoa au lini mtatembelea wazazi
wako na kadhalika. Kukandamiza hoja mara nyingi kwa mwanaume huonekana kama
dharau. Asilimia 96% ya wanaume waliohojiwa wanasema kuwa mwanamke anakuwa
mkandamizaji wa hoja pale anapotaka mwanaume afanye jambo fulani ambalo
tayari mwanaume anajua anatakiwa kufanya
hivyo na hilo kwa wanaume ni usumbufu mbaya. Utafiti uliofanywa na DR. HOWARD
MARKHAM wa kituo cha Marital and family huko DENVER MAREKANI unaonyesha kuwa
ukandamizaji wa hoja una nguvu sawa na uzinzi katika uvunjaji wa ndoa. Mwanamke
anayeamini kuwa asiporudia kumwambia mumewe jambo fulani mumewe hatafanya na
marudia hayo yatamfanya mwanaume ajione
kama mtoto na huzaa chuki.
9. WIVU MCHAFU
Wivu
huonekana pale ambapo mwanamke anahofu kuwa huenda mpenzi wake ataanzisha
uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine hasa iwapo mwanamke mwingine mzuri
kuliko yeye anakuwa karibu yake. Wivu unakuwa mchafu pale ambapo hakuna sababu
dhahiri ya mwanamke kumshuku mumewe. Mwanamke wa aina hiyo anafanya kama vile
mwanaume ni mali yake. Utakuta mwanaume anaulizwa maswali mengi mno kama vile
yupo Kituo cha polisi Nyendo za mwanaume kufuatiliwa kwa karibu sana na mara
nyingine hufikia kukatazwa kuwa karibu na watu au marafiki fulani. Mara nyingi
mwanamke huyo akiambiwa kuwa ana wivu hukana na kuhalalisha tabia zake kwa
visingizio mbalimbali. Hayo yote ni machukizo makubwa kwa mwanaume.
10.
WAONGEAJI
KUPITA KIASI
Ni
kweli kuwa wanawake wameumbwa kuwa waongeaji na ndio maana tafiti zinaonyesha
kuwa wanawake ni wepesi zaidi wa kujifunza lugha mpya kuliko wanaume. Katika
sayansi ya mapenzi inakadiriwa kuwa mwanamke anaweza kuongea maneno 20,000 kwa
siku wakati mwanaume uwezo wake unakadiriwa kuwa na maneno 7,000 tu kwa siku.
Mwanamke aongeae kupita kiasi mara nyingi anakuwa hajijui kuwa ni tatizo kwani
yeye mwenyewe anajiona kuwa kama mtoa burudani mzuri kumbe bila kujua anawaboa
wengine. Mara nyingi mwanaume anapata shida kumkatisha na mara nyingine
anaogopa kumkatisha ili asije akamkasirisha mpenzi wake. Kwa kuwa mwanamke huyo
ni muongeaji sana utakuta mpenzi wake tayari anajua mambo mengi ambayo mwanamke
huyo hupenda kuongelea na pia anajua mitazamo yake juu ya mada mbalimbali hivyo
urefu wa maongezi yake mara nyingi inakuwa kero iletayo chuki. Muongeaji huyu
wa kike tayari atakuwa anafahamika kwa marafiki wa mwanaume huyo na hivyo
marafiki wa mume watakuwa wanamkwepa rafiki yao pale wanapojua atakuwa na mke
wake (au mpenzi wake), hilo ni pigo kwa mwanaume. Marafiki hao watamwogopa
mwanaume huyo kwani wanajua akiwepo mkewe basi bomba la mazungumzo marefu
litang’oa masikio yao.