Wednesday, June 8, 2016

JINSI VISINGIZIO VINAVYOHARIBU PENZI


Mwanadamu ameumbwa na kiu kubwa ya kupenda kuwa sahihi, kuonekana anaweza na pia kujiona kuwa anafaa na kukubalika. Kutokana na ukweli huo Mwanadamu anajiona kuwa anao wajibu wa kufanikiwa na kukubalika kutokana na mafanikio ayapatayo katika maeneo mbalimbali katika maisha yake. Hatari iliopo kwa kila mwanadamu ni pale anapojikuta ameshindwa kufanikiwa na ili asijilaumu  yeye mwenyeawe anamsingizia mtu mwingine au mazingira aliyopo. Mwanadamu wa kwanza kushindwa kutii amri aliyopewa  na Mungu nakula tunda walilokatazwa alitoa kusingizio kwa kushindwa kutii amri aliyopewa  hebu msikilize hapa,“ Adamu akasema, Huyo Mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala Bwana Mungu akamwambia mwanamke Ni nini ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya nikala” Pamoja na visingizio walivyotoa wazazi wetu wa kwanza adhabu walipewa na Mungu mwenye haki. Kwa maneno mengine ni kwamba ukosefu wa umakini au uangalifu lazima utatuletea majanga ya aina fulani kwani ni wajibu wetu kujitahidi kuepuka makosa au kushughulikia madhaifu tuyaonayo katika mahusiano yetu.

Kuna sababu mabalimbalil zinazopelekea mtu kutoa visingizio lakini wengi hutoa visingizio kwa sababu zifuatazo.
1.    Kuogopa kufikiriwa vibaya
2.    Kuogopa kushindwa
3.    Kuogopa mabadiliko
4.    Kuogopa kuwajibika
5.    Kuogopa kufanya kosa
6.    Kuogopa ugomvi
7.    Kuogopa kuonekana hujui au huwezi.

Watu wanaotumia visingizio mbalimbali kuhalalisha matatizo au madhaifu yao hawajui kuwa wanajikosesha fursa ya kujifunza mambo mapya na kutatua matatizo yao na hivyo kutengeneza mazingira mazuri ya kimapenzi.

Vifuatavyo ni visingizio mbalimbali ambavyo wapendanao hutumia kuharibu ubora wa husiano wao.

1.   SINA MUDA WA KUTOSHA
Mwanzoni mwa mahusiano ya kimapenzi utaona wazi kuwa mpenzi wako anafanya jitihada kubwa za kutafuta muda wa kuwa na wewe au kuongea na wewe kwenye simu lakini baada ya muda fulani unasikia mpenzi yule yule anasema kuwa ana kazi nyingi ( yuko bize) na hana muda wa kuwa na wewe au kuongea na wewe.Hivi karibuni nimesikia kisa cha dada  ambae mpenzi wake aliemzoesha kumpigia mara kwa mara na baadae kuacha  kufanya hivyo, kaka huyo alitoa kisingizio cha kukusa salio la muda wa hewani na dada huyo alipofuatilia aliona ni ukweli kwani biashara ya kaka huyo ilikuwa na hali mbaya.Nilifurahi kusikia kisingizio hicho toka kwa mwanaume kwani kwa sehemu kubwa wanawake wengi  ni sugu katika kutumia kisingiizio hicho .Swala la mtu kutumia kisingizio cha ubize mara kwa mara ni dalili ya penzi kunyauka. Uonapo hilo limeanza kujitokeza tambua kwa hakika kuwa penzi lake kwako  limeanza kubadili muelekeo na huko linakoelekea  ndiko  alikokazia macho yake na sio rahisi kukukumbuka wewe. Iwapo utaamini hilo na mtu huyo bado anadai yupo bize nab ado anakupenda basi tambua unayokazi ya kuleta mabadiliko ili mrudie hali ya mwanzoni. Hebu fikiria yafuatayo kwa mtu anaesema yuko bize, Iwapo tuko bize sana tukashindwa hata kupika chakula – tutakufa njaa. Iwapo tuko bize sana tukashindwa kufanya usafi wa miili na nyumba zetu tutanuka na kupata magonjwa. Kwa maneno mengine mpenzi wako naposema yupo bize mara kwa mara maana yake ni kwamba haoni uthamani wa uhusiano wenu na hajali iwapo utaharibika kwa ukosefu wa muda wa kujenga na kuimarisha uhusiano wenu.

Hebu fikiria mfano mwingine, mtu anasema “ napenda sana kujisomea BIBLIA au Quran lakini nakosa muda wa kujisomea” Je mtu huyo huyo iwapo anatumia muda mrefu kuangalia TV au Kuchat na marafiki zake kweli utasema kweli anapenda kusoma BiBlia au Quran?

 Kila mmoja wetu ana masaa 168 kila wiki na iwapo unatoa kipaumbele kwa mpenzi wako lazima uamue kupunguza mambo mengi ila ufanya mambo ambayo yatamthibitisha mpenzi wako kuwa ni wa muhimu kwako.KWA mtu anaekupenda lazima atoe kipaumbele kwako kwa kuweka mabo mengine pembeni.Kuelewa vizuri maneeno yangu fikiria juu ya mzazi kuacha starehe ya pombe ili  fedha zitumike katika kusomesha mtoto wake,au pale unapomnunulia mpenzi wako zawadi haimaniishi kuwa fedha unazotumia hazina kazi kwa upande wako bali unataka umfurahishe mpenzi wako.




2.   VISINGIZIO VYA KUTOJUA
Watu wengi wamekuta mahusiano yao yanaharibika kwa kuwa hawakufanya bidii kufahamu mambo mengi juu ya wapenzi wao na hivyo kusubiri kuambiwa kila kitu. Unaposubiri uambiwe kila jambo unamboa mpenzi wako. Nakumbuka siku moja kupokea sms toka kwa mpenzi wangu na ilikuwa jioni ambapo nilikuwa  nimechoka na sikupenda kujibu kwa sms. Nilimpigia mpenzi wangu na simu haikupokelewa na  ukapita muda hakunipigia, baadae kidogo kanibip, nikachelewa kumpigia kwa kuwa nilikuawa naongea na simu nyingine, nilipomaliza nikampigia kwa mara ya pili tena simu haikupokelewa. Baadae nilipoonyesha kuwa nimekasikirika kwa yeye kushindwa kupokea simu yangu akasema kuwa “ Yeye alijua kuwa meseji yake ningeijibu kwa meseji na hakujua kuwa ningepiga badala yake. Niliumia na kumuuliza, “Je, tumewekeana mkataba kuwa sms lazima ijibiwe na sms” akasema, hapana .Ndugu yangu unaona kisingizio alichotumia mpenzi huyo? Anasema alikuwa hajui kuwa upo uwezekana wa mimi kupiga baada ya kukuta sms yake. Je kisingizio hicho kitasaidia kujenga penzi au kubomoa?

Kuna watu wengi wanaleta utani unaofanana na ukweli na mpenzi anapokasirika kutokana na utani huo hujitetea kuwa “ nilikuwa sijui kuwa itakuumiza hivyo” Mtu mmoja ambae alikuwa anachukia watu wanaotumia visingizio alisema hivi. Mimi huvunja uhusiano haraka sana. Sitaki nizeeke kwa kumwelezea mtu mzima wapi ananiboa” Mtu huyo anaonyesha ni jinsi gani uzembe wa aina yoyote ni kosa la jinai kwake.Ni muhimu ndugu yangu ujitahidi kuwa makini kwani haiwezekani kuwa mpenzi wako atakuambia kila kitu anachohitaji au kukichukia, ni juu yako kuonyesha penzi la kweli kwa kujitahidi kuongezea maarifa ili uwe bingwa katika kila eneo la uhusiano wako.Itakuwa rahisi kwa penzi kati yenu kuongezeka iwapo mtajenga mazingira ya uwazi a,\mbapo unajisikia huru kuuliza maswali mbalimbali.


3.   VISINGIZIO VYA KIFEDHA
Kwa sehemu kubwa mahusiano ya kimapenzi huhusisha fedha katika maeneo mbalimbali, muda wa maongezi kwa njia ya simu, gharama ya vyakula na vinywaji, zawadi za hapo na pale na mahitaji mengine muhimu. Tafiti zinawaonyesha kuwa pale mpenzi mmoja aonapo mwenziwe anatumia fedha vibaya kiwango cha penzi na furaha kati yao hupungua. Hebu fikiria ukweli wa  utafiti huo, Je sio kweli kuwa mke ambae anamwona mume wake kuwa hawezi kulala bila kunywa pombe ataongezeka furaha au furaha itapungua, Je mume anaemuona mke wake anapenda kununua nguo za bei mbaya kila mwisho wa mwezi je furaha yake itaongezeka au itapungua? Ni muhimu uone kuwa kupungua kwa furaha kwa mmoja kutaathiri uwezo wake wa kuonyesha

penzi motomoto na hivyo kuweka uhusiano wenu katika eneo la hatari. Eneo lingine la kifedha ambalo ni hatarishi ni kuficha matumizi makubwa au matumizi yasiokubalika. Mtu atapewa Ths. 50,000/= kwa ajili ya mahitaji muhimu anatumia Tsh. 40,000/= na nyingine anatumia kwa matumizi yake binafsi. Anasema sina hela kumbe anazo na anaziweka kwa ajili ya matumizi haramu. Watu wengi hutumia visingizio mbalimbali kuhalalisha kutotumia fedha zao kwa ajili ya wawapendanao au kujifanya hana fedha ili kumnyonya mwingine. Visingizio hivyo  unaweza kuvitumia na kujiona mjanja kumbe mwenzio anajua unamdanganya na visingizio vyote utumiavyo ni uongo mtupu. Kwa kuwa mpenzi wako hataweza kukuambia juu ya hisia zake juu ya matumizi yako ya fedha au utegemezi wako wa fedha kwake ,taratibu penzi kati yenu linanyauka  hadi kufa  Kabisa.

VISINGIZIO VYA KURUHUSU MAOVU DHIDI YAKO YAENDELEE.
Sikatai kwamba ni kweli mara nyingine mpenzi wako kweli kabisa anakuwa na kazi nyingi kuliko kawaida  lakini kamwe usianze kumtetea ili kuhalalisha visingizio vyake iwapo unaona wazi kuwa iwapo angefanya bidii lazima angepata muda wa kukuonyesha wewe kuwa ni mtu wa muhimu katika maisha yake. Mtu anakwambia yuko bize kweli kama kweli anakupenda hawezi kuamka saa 8 za usiku na kukutafuta, ndio anatumia kisingizio kuwa amechoka na kazi na hamuwezi kucheza  ngoma ya wakubwa je kweli haweza kujitolea akakuamsha saa 9 usiku mkacheza ngoma hiyo? Ukishindwa kumkabili na kumwonyesha ulemavu wa kisingizio chake utaendelea kujidanya kuwa unapendwa kumbe mwenzi ameshakuwa msagaji au shoga. Tambua kuwa nyuma ya kila kisingizio kunasababu usioambiwa ya yeye kusema hivyo. Usiruhusu mpenzi wako aamini kuwa utakubaliana na kisingizio chochote anachotoa.

Iwapo unajikuta unakubaliana kwa urahisi na visingizio vya mpenzi wako tambua kuwa uko katika uhusiano ambayo kamwe hutaweza kuwa na furaha ya kudumu. Ni kweli kabisa kuwa unampenda sana  mpenzi wako anaekuumiza lakini ni muhimu ukumbuke kuwa hustahili kuwa mtu wa kuumizwa umizwa mara kwa mara haswa na mtu anaendai kuwa anakupenda. Sio hilo tu na hata pale ambapo unajikuta una mpenzi anaeboa mara kwa mara na moyoni unaona kuwa kwa uhusiano wa muda mrefu mtu huyu hafai ,ni vyema kusikiliza moyo wako badala ya kutafuta visingizio vya wewe kuendelea na uhusiano usiiokusisimua kama unavyotamani iwe. Ni kweli hajakufanyia uhalifu mkubwa lakini iwapo haonyeshi bidii ya kuleta uchangamfu na raha unayohitaji ni wakati wa kufikiria upya juu ya uhusiano huo. Bila shaka umeshawahi kusikia mtu akisema, “Akiwepo fulani nyumba inachangamka sana.” Maneno hayo ni ushahidi kuwa uchangamfu ni wa muhimu sana miongoni mwa wapendanao.
   
Ndugu yangu, ni wakati wa kupiga vita visingizio vyoyote  anavyotumia mpenzi wako kukukosesha raha na wewe mwenyewe upigi vita visingizio vinavyomkosesha raha mpenzi wako.Katika utafiti uliofanyika huko UINGEREZA  na shirika la sheria liitwalo Slater and Gordon  UNAONYESHA KUWA watu wengi hubakia kwenye mahusiano yanayowaumiza kwa visingizio vya aibu ya kuachwa,woga   wa kubakia bila mpenzi  au woga wa kukosa fedha   walizokuwa wanapata kwa mpenzi huyo mtesaji.Ni wakati sasa wa kuangalia upya kiwango cha furaha kati yenu kama kinaridhisha, kama hakiridhishi angalia nia aina gani ya visingizio vinatumika kuendeleza maumivu kati yenu na kupambana na visingizio hivyo kikamilifu. 




PENZI LINAPOGEKA KUWA KERO

Mahusiano ya kimapenzi ni kitu kizuri sana ndio maana mara ya kwanza mtu anapoingia katika mahusiano ya kimapenzi anakuwa na furaha kubwa sana. Naomba uzingatie kuwa nimesema kuwa mtu anapoingia  katika uhusiano kwa mara ya kwanza, yaani  kama ni mwanaume huyo anakuwa ndie mwanamke wa kwanza kabisa kwake    na   kwa mwanamke huyo ndio  anakuwa mwanaume wa kwanza kabisa. Katika ulimwengu tulionao sasa ni mara  chache sana utaona kuwa mwanaume ambaye hajawahi kuwa na mahusiano ya kimahaba  NA MWANAMKE anaanza na mwanamke ambaye na yeye huyo ndio anaekuwa mwanaume wa kwanza.

Tatizo tulilonalo sasa utakuta mwanaume ambaye tayari ameshakuwa na mahusiano na wanawake 2 anaanza uhusiano na dada ambaye hajakuwa na uhusiano wowote au dada ambaye ameshakuwa na mahusiano na wanaume wawili anaanza mahusiano na mwanaume ambae hajawa katika mahusiano ya kimapenzi.Katika mazingira kama hayo lazima mtu atajikuta analinganisha mpenzi aliene sasa na Yule aliemtangulia.

Katika kazi yangu katika Clinic ya afya ya mapenzi huu ni mwaka wa kumi toka nianze vipindi redioni na mara chache katika TV na asilimia zaidi ya 95% ya wateja wanaofika ofisini kwangu ni wanaume na asilimia kati ya 30 hadi 40ni wanawake .Asilimia kubwa ya wanaume wanaokuja ofisini kwangu wana matatizo ya nguvu za kiume au kuwahi kumaliza upandaji wa mbegu dume.

Vilio vingi  toka kwa wanawake ni kutoridhika na raha wanayoipata katika uchezaji wa ngoma ya wakubwa na ukosefu wa penzi wanalohitaji na hasa kushuka  kwa mawasiliano na muda wa kuka pamoja. Wakati wanaume wanalalamika kuwa wanawake wanawanyima haki zao za kucheza ngoma ya wakubwa wanawake wanalalamika kuwa hawafurahii kucheza ngoma ya wakubwa na wapenzi wao.BILA shaka hapo unaweza kuona chimbuko l mvutano unaotokea katika mahusiano mengi ya kimapenzi.

Tafiti baada ya tafiti zinathibitisha kuwa udhaifu au uzembe katika kucheza ngoma ya wakubwa unachangia sana katika migogoro inayojitokeza katika mahusiano ya kimapenzi na zifuatazo ni SMS toka kwa wasikilizaji wangu wa redio, SMS, ambazo zinaonyesha jinsi gani penzi linaweza kugeuka kuwa kero kubwa
 ‘Dr. Nelson mimi ni kijana wa umri wa miaka 25 nimekuwa na mahusiano na dada mmoja na huu tunaingia mwezi  wa 3 cha ajabu ni kwamba dada huyo hakuwahi kuniambia kuwa ameolewe na nikajikuta nampenda sana huyo dada.

Sasa nimegundua  kuwa ni mke wa mtu na  nashindwa kumuacha japo na mimi nina mchumba. Sasa Dr. huyo mke wa mtu anataka azae na mimi jambo ambalo linanichanganya akili na kuniletea kishawishi cha kufanya jitihada nivunje ndoa yake nimuoe yeye Dr. nifanyeje?.”

“Dr. Nelson mimi naitwa Issa nina umri wa miaka 29 nimeoa toka mwaka juzi. Tatizo ni kwamba kila nikimwambia  mke wangu kitu cha maana kama hajakipenda huniambia nitaenda kuolewa na mwanaume mwingine kwani mwanaume sio wewe peke yako, mbaya zaidi wakati wa kucheza ngoma ya wakubwa yaani hata kabla sijamaliza ananiambia toka mimi nimechoka na mimi kulazimika kumaliza haraka haraka. Dr. hali hiyo inanichukiza sana naomba unisaidie hali hiyo inasababishwa na nini?.”

“Kwa jina naitwa Joyce niliishi vizuri na mume wangu ikafika sehemu akaona simtoshelezi na akanisaliti na kuniambukiza magonywa ya zinaa mara 2. Hayo yakanifanya niende nje ya ndoa ili nipata kujua nina  utamu au uchungu, nikashangaa napewa sifa kibao n huduma kupewa nikaanza kumnyima mume wangu unyumba na kuacha aendelee na dogo dogo.”

“Dr. mimi niko kwenye ndoa mwaka wa 11 mke wangu hunipa unyumba kwa shingo upande. Pia ameshanitamkia kuwa hanipendi mimi nampenda Dr. nifanyeje ili upendo urudi?.”

“Dr. Nelson asante sana kwa mafundisho yako ambayo yanatupa tumaini kuwa upo uwezekano wa mtu kufurahia ndoa siku zote. Niko ndani ya ndoa na nina tatizo. Toka niolewe na mume wangu ninapomsemesha anakuwa mkali na akiwa nyumbani ni kimya hamna mazungumzo na mara nyingine yuko bize na simu. Siku akikusemesha vizuri ujue anataka umpe ngoma ya wakubwa acheze unanishaurije hapo?.”

Kesi ya kwanza ni ya mwana mke aliechepuka kwa kijana ambae hajaoa na akajikuta amekolea penzi mpaka anataka atengeneze kumbukumbu  ya utamu aliopata kwa kuzaa na mwanaume mwingine na kesi ya pili ni ya mwanamke ambae hampendi mume wake na si ajabu  ana mchepuko. Je ni mambo gani ambayo yanachangia katika kuleta mikorogano mbalimbali miongoni mwa wapendanao? Najua yapo mambo mengi sana kama matatizo ya kifedha, uchafu, wivu, ndugu, unene na ukosefu wa uwazi na maongezi ya kutosha baina ya wapendano pamoja na madhaifu katika utendaji wa tendo la ndoa. Lakini kwa kuwa sayansi ya mapenzi inathibitisha kwa kati ya asilimia 80% hadi 85% ya migogoro yote katika ndoa chimbuko lake ni hitilafu katika kucheza ngoma ya wakubwa upo umuhimu wa kuangalia eneo hilo kwa makini sana.

Ni vyema tuangalie eneo hilo kwa upya na kwa umakini mkubwa sana. Mwanzoni mwa  uhusiano kwa wengi kila kitu ni kipya na chenye uwezo mkubwa wa kuleta msisimko mkubwa na  mmoja au wote hupenda hali hiyo tamu iendelee milele. Lakini kwa bahati mbaya mwanamke atapata shida kufika kileleni iwapo atakuwa katika mazingira ambayo yanamletea huzuni, wasiwasi, kutojiamini, hasira au kuwa na hali ya kujiona kama mtu alieshindwa.
Mwanamke atajiona kama mtu alieshindwa pale anapojiona kuwa ni mnene na hataki unene, pale anapojiona kuwa hana fedha za kufanya hili na lile kama marafiki au majirani wanavyoweza kufanya na mbaya zaidi akiwa na mume ambaye hawi karibu na yeye mara kwa mara inatengeneza uchungu nafsini mwake.
Mwanaume anaposhindwa kuwa karibu na mpenzi wake mara kwa mara mwanamke hujisikia vibaya kwa kuwa anajiona kama hana mvuto mkubwa sawa na yule mama aliechepuka, na huko kwenye mchepuko akajikuta anasifiwa na kuonyeshwa kuwa ni mtu wa muhimu kwa mafunzo aliopata mchepukoni.
Kama ulivyoona kwenye stori hiyo mama huyo baada yakupata mchepuko aliona uhalali wa kumnyima unyumba mume wake na moyo wake usimhukumu kabisa.
DR. David Barlow wa chuo kikuu cha Boston huko Marekani katika utafiti wake wa kina ameshuhudia kuwa mwanamke ambaye huko nyuma ameshawahi kuwa na mwanaume mwenye matatizo ya nguvu za kiume au kuwahi kumaliza au kukosa hamu ya tendo la ndoa, anapojikuta mume aliyenae sasa ameanza kuonyesha madhaifu kama hayo hiyo inamzuia mwanamke huyo kulainika na kutokwa na vichocheo ambavyo vingemuwezesha afike kileleni kwa urahisi na hivyo kumuona mumewe kuwa mwanaume wa ukweli.
Mbaya zaidi ni mwanamke ambaye mpenzi wake anaonyesha kuwa anataka apate uhakika kuwa mpenzi wake wa kike amefika kileleni. Mwanamke anapokuwa na mwanaume anaemtia presha ili afike kileleni na yeye anajikuta hisia zake zinabadilika na kuwa tendo la ndoa kama kero fulani.
Hapo mwanamke huyo ataanza kudanganya kuwa amfika mahali ambapo hajafika. Utaweza kuona uzito wa kero hiyo katika mesiji iliotoka kwa dada mmoja isemayo hivi :
“Dr. Mimi napendwa na wanaume wawili na tatizo nililokumbana nalo ni kwamba yule nisiempenda ndie ambae ananipa raha kubwa ninapocheza nae ngoma ya wakubwa lakini huyu ninaempenda japo ana fedha nyingi anaponihitaji kimapenzi naona kama usumbufu. Dr. nifanyeje nibadilishe hali hiyo?”
Meseji hii inathibitisha kabisa utafiti wa Dr. DAVID Barlow niliemtaja hapo juu kuwa mwanamke ambaye tayari ameshakuwa na mpenzi kabla yako anapokulinganisha na mwanaume aliekutangulia anakosa amani lakini hatakuambia hilo na kujikuta anakuwa na huzuni mara kwa mara.Mbaya  zaidi  hali hiyo  ikiendelea inaleta hasira kama dada mmoja alivyonisimulia..
    “DR.NIKO kwenye ndoa mwaka wan ne mume wangu ananipa kila kitu ninachohitaji bila kujali bei  yake lakini kwenye tendo la ndoa ni mvivu na mara nyingine ananikewepa.NILIKUWA NAMPENDA SANA  lakini kutokana na hali hiyo katika eneo la ngoma ya wakubwa nimejikuta nimeanza kumchukia.DR. UTANISAIDIAJE NIBADILISHE hali hiyo?  “








Tatizo la wanawake kukosa hamu ya tendo la ndoa ni kubwa sana na linachangia kuharibu furaha katika mahusiano mengi ya kimahaba. Tafiti ya hivi karibuni inaonyesha kuwa moja ya tatu ya wanawake wenye umri kati ya miaka 18 – 59 wanakosa  hamu ya tendo la ndoa. Ni muhimu kutambua kuwa hamu ya tendo la ndoa ni tofauti  kabisa na uwezo wa mwanamke kujisikia raha ya tendo la ndoa wakati linatendeka. Unaweza kuona kama jambo ambalo haliwezekani lakini tafsiri zinathibitishwa kuwa wapo wanawake wengi ambao wanajishangaa kuona hawana hamu ya tendo la ndoa lakini wanapojitoa muhanga na kufanya mchezo huo hupata raha hadi kufika kileleni.

Kiongozi wa ufatifi huo Profesa Alan Rilely wa chuo anasema kuwa ukweli huo wa kisayansi bado unaonekaa sana miongoni mwa wanawake kati ya umri wa miaka 18 – 54 mwanamke anapojitoa kumpa penzi mumewe ataweza kufika kileleni iwapo mumewe huyo anayo maarifa ya kutosha katika kumwandaa mkewe  kabla ya yeye kupanda jukwaani na pia awe na uvumilivu wa kutosha kutumia muda mrefu katika kumwandaa  mkewe.

Mwanaume atumiapo muda mrefu katika kumwandaa mwanamke anasababisha mwanamke atokwe na kichocheo kingi cha OXIYTOCIN kichocheo ambacho hupunguza makali ya kichocheo kilelecho hicho kiitwacho CORTISOL. Kupunguzwa kwa makali ya uchovu kunamruhusu mwanamke aanzzw kupata raha japo mwanzoni alikuwa hana hamu ya kucheza ngoma ya wakubwa. Katika hili ushahidi toka kwa mke wangu mwenyewe ambaye aliweza kufanya kukataa kucheza ngoma ya wakubwa lakini nilipomchombeza akajikuta anafurahi na tukaweza kucheza midundo mingi ya ngoma ya wakubwa. Kutokana na hali hiyo kujirudia mara nyingi mke wangu siku moja aliniambia kuwa kusema maneno haya “usingekuwa unapenda dini wewe ungekuwa muhuni sana”

Kwa wanawake wengi ukosefu wa ukaribu wa kutosha na wapenzi wao husaidia wapoteze hamu ya tendo la ndoa jambo ambalo wanaume wengi hawajui pale wanapojikuta wananyimwa nafasi ya kucheza ngoma wanayoipenda sana. Ukosefu wa ukaribu unapunguza mshikamano wa kihisia cemotional connection) na kumfanya mwanamke amwone mwanaume kama mzigo badala ya kumuona kama sehemu yake mwenyewe utatambua kuwa mpenzi wako anakuwa kama mzigo pale uonapo anakuwa mzito kukubaliana na wewe katika maeneo mbalimbali ikiwamo kucheza ngoma ya wakubwa.

Wanaume wengine nao huwa vimeo na kupata shida kukubali kuwa wamepoteza hamu ya tendo la ndoa na hivyo kusababisha wake zao au wapenzi wao wa kike kuamini kuwa lazima watakuwa na mchepuko. Mwanamke anapoona kuwa mumewe au mpenzi wake hana hamu na yeye na kuamini kuwa ana mchepuko japo hana ushahidi wowote ni rahisi kwake kukubali kuingia katika  ulimwengu wa michepuko. Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale ambapo mwanamke ana hamu na mumewe na mumewe hana hamu na mke wake, katika hali kama hiyo kwa kuwa mwanaume hataki aonekane kama kimeo (asieweza kazi ya kiume) anakuwa mkali kwa mkewe. Hali hiyo imejirudia mara nyingi unakuta mwanaume anakuwa mkali  kwa mkewe katika makosa au madhaifu madogo madogo jambo ambalo humuumiza sana mkewe. Maumivu hayo ya mwanamke yanamfanya awe mouongo kufuatilia akili yake ya kimapenzi na hivyo kutengeneza hali ya mchepuko.

Katika mazingira kama hayo hata pale mwanaume atakapokuwa na hamu na mkewe na mkewe atakuwa katika hali ya ukavu kutokana na uvhungu uliosababishwa na ukali wake yeye mwenyewe. Mwanamke huyo anapojikuta anakuwa mkavu kwa mumewe jambo ambalo halikuwepo kabisa anashindwa kukubali kuwa sasa tayari amekuwa kilema katika eneo hilo na hivyo kujaribu kucheza na mwanaume tofauti. Kilichonisababisha kuandika mada hii ni kutokana na simu mbili toka wanawake wawili tofauti ambao wamejikuta sio vilema baada ya kuchepuka nje ya ndoa zao. Kujiona kuwa sio wa kutamanika, kujivunia maumbile ya mwili wako ni jambo la muhimu sana katika kusababisha vichocheo vya hamu ya ngoma ya wakubwa kufanya kazi vizuri.

Ukiwa mnene, matiti madogo au bunduki ya kiume ndogo,  makalio madogo au mfupi wa kimo, ukiwa mweusi na unatamani ungekuwa mweupe hayo yanapoingia akilini mirija ya vichocheo inasinyaa  kushindwa kuleta mtiririko mzuri wa  hamu ya ngoma ya wakubwa.  Pale mtu anapojiona kuwa hana maumbile ya kutamanika anajikuta hafikirii sana juu ya raha ya tendo la ndoa, mtu anapokuwa hafikirii mara kwa mara  juu ya tendo la ndoa anashindwa kutengeneza  kiwango cha kutosha cha kichocheo cha TESTOSTERONE ambacho husababisha hamu ya tendo la ndoa miongoni mwa wake kwa waume.

Utafiti wa miaka 33 unaonyesha kuwa asilimia 15 ya wanawake wanaotumia vodonge vya majira kuzuia kupata ujauzito wanapoteza hamu ya kucheza ngoma ya wakubwa. Kiongozi wa utafiti huo daktari bingwa wa mambo ya wanawake (GYNECOLOGIST) Dr. Lee sharman anasema wanawake wengi wanasingizia idonge hivyo jambo ambalo sio la kweli. Utafiti huo uliohisisha wanawake 8,400 ulionyesha kuwa asilimia 22 hamu ya tendo la ndoa  iliongezeka, asilimia 63 hawakuona badiliko lolote lile na ni asilimia hiyo 15 tu ndio walioona upungufu wa hamu ya tendo la ndoa.

Dr. Lee anasema wanawake hao huona hicho kuwa kisingizio rahisi  kwa kuwa hawataki kuangalia maeneo mengine yenye uwezo mkubwa wa kuwapunguzia hamu ya tendo la ndoa kama woga  wa kuhoji mambo, kuogopa migogoro, ukosafu wa uwazi, kushindwa kumweleza mwanaume kuwa ameshindwa kazi ya kiume au ana maumbile madogo na kadhalika.

Uhusiano wa kimapenzi unahusu mambo mengi kama maongezi, fedha, usafi, zawadi kukosoana na sio tendo la ndoa peke yake lakini ukiondoa tendo la ndoa mengine yote yanakosa nguvu  za kushiriki uhusiano wa kimapenzi. Tatizo ni kwamba watu wengi hawajui kuwa tendo la ndoa linaweza kuongezea  nguvu mambo mengine na hivyo kufanya bidii kubwa katika hilo. Tatizo ni kwamba ukifanya bidii katika eneo hilo na ukapuuzia maeneo mengine utakuwa unatengeneza upinzani wa wewe  kufurahia tendo la ndoa toka  kwa mwenzio japokuwa anakupenda. Na sio hilo tu bali pia ukifanya bidii katika maeneo mengine na kupuuzia tendo la ndoa lazima utazua mgogoro kati yenu.

Watu wengi wanashindwa kuwa makini katika maeneo mengi ya kimahusiano lakini ni wepesi sana kulaumu pale mpenzi anapomwacha au kumsaliti. Ni kweli kabisa kuwa mwisho wa uhusiano unaumiza sana bila kujali nani amesababisha hilo lakini wengi hawachukui tahadhali. Unaweza kusema kuwa hata ungefanya nini kama mtu atakuacha atakuacha tu, hivyo ni kweli lakini pale unapoachwa

JE NGOMA YA WAKUBWA YAWEZA KUVUNJA NYUMBA?
Tunaposikia watu maarufu hasa wasanii wamevunja mahusiano yao huwa tunashangaa sana kwa kuwa hao ni watu wenye fedha nyingi sana na kutokana na umaarufu wao usingetegemea hali hiyo kutokea. Mara nyingi tunasikia kuwa usaliti, ulevi au fedha ndio vitu vinanvyochangia ndoa nyingi kuvunjika lakini hatusikii kuwa matatizo ya nguvu za kiume, ukubwa wa maumbile au udogo wake au ukosefu wa ufundi wa kutosha katika uchezaji wa ngoma ya wakubwa kuwa ni visababisho ukweli ni kwamba madhaifu katika eneo la tendo la ndoa yamewaleta wengi sana katika ofisi yangu.

Mwanzoni mwa uhusiano mara nyingi kila mmoja anajiona kuwa ni mwelewa na yanakuwepo matarajio kuwa huenda madhaifu hayo yatatokomea baada ya muda Fulani jambo ambalo kwa wengi halitokei. Pale inapokuwa wazi kuwa tatizo halitatokomea, huzuni na hali  ya kukweka kushiriki kucheza ngoma ya wakubwa wanatokea. Hali hii humfanya mmoja au wote wawili kujisikia upweke ndani ya nafsi yake na upweke huo hubadilika kuwa uchungu na mwishowe kuwa hasira. Inapotokea kuwa ni mmoja ambaye ana tatizo, fedheha na kujiona kama kimeo itasababisha awe mkimya au atumie ukatili kumkwepa mpenzi wake anayependa wacheze ngoma ya wakubwa mpenzi ambaye hana tatizo atajisikia vibaya kuomba apewe kitu ambacho mpenzi wake hapendi kukitoa.

Hali hiyo isipotafutiwa ufumbuzi yule asie na tatizo ataanza kuwa mtu mwenye hasira katika maeneneo mengine tofauti na ngoma ya wakubwa. Hatari ni kwamba tatizo hilo linapokuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu linasababisha mmoja kujitenga kihisia na kuonekana hana uchangamfu uliokuwepo mwanzoni. Mpenzi anapojitenga kihisia kutokana na kero ya kunyimwa anachokipenda na mtu anayedai kuwa anampenda inakuwa vigumu sana kurudia hali ya uchangamfu ule wa mwanzoni.

Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 43 ya ndoa zinazovunjika mzizi wake ni udhaifu au ujinga katika kucheza ngoma ya wakubwa na watafiti hao wanasema kuwa idadi inaweza kuwa kubwa zaidi ya hiyo kutokana na wengi kukwepa kukubali kuwa wameshindwa kucheza vizuri. Kiongozi wa utafiti huo Dr. Sari Eckler Cooper anasema kuwa pale uonapo ndoa inavunjika kutokana na usaliti ni kwamba yule aliechoka kutokana na kunyimwa mchezo au kutoridhika na utamu wa ngoma ya wakubwa anaamua kusaliti ili  asababishe kuachana na yule anaemuona kuwa kimeo katika kucehza ngoma  ya wakubwa. Watu wengi wanadai kuwa jambo kubwa linalosaidia kudumisha ndoa ni uvumilivu na mimi napingana na jambo hilo japo naamini kuwa uvumilivu ni jambo zuri. Unapovumilia jambo lazima liwepo tumaini kuwa hali hiyo itabadilika kwa  kuona bidii ambayo mwenzio anaifanya kuleta mabadiliko. Iwapo mpenzi wako alien a udhaifu Fulani anafahamu jinsi udhaifu wake unavyokukosesha raha na  asifanye bidii ya kuleta mabadiliko huo ni ukatili mkubwa usiohitaji uvumilivu kabisa kutokana na imani yangu hiyo kuwa lazima uvumilivu uwe na mpaka nilijikuta siku moja nasema kitu ambacho hata mimi mwenyewe kilinishangaza.

Dada mmoja katika ofisi moja alisema “Ndoa ni kuvumiliana” na mimi haraka sana nikasema “Kuvumiliana kumewekewa mbwa, mbwa wanapofanya mapenzi wanafuatana na hata ukipiga mbwa jike na mbwa dume haachani wanavutana pamoja na kubakia wemenatana hivyo”. Baada ya kutamka jambo hilo ambalo lilikuja bila kupanga nilijikuta nimeanza kufikiria juu ya ukweli wa lile nililosema. Mbwa wanajikuta katika hali hiyo lakini hali hiyo haidumu siku nzima kwani baada ya muda fulani huachiana jambo ambalo linatupa picha ya kwamba unapovumilia jambo lazima liwepo tumaini ya hali kubadilika na kuwa kama ile ya mwanzoni kinyume na hivyo ni gereza la mateso.

Upo uwezekano mubwa wa mwanamke kupungukiwa na hamu ya tendo la ndoa baada ya kujifungua jambo ambalo linatoa mwanga kwanini raha ya ndoa hupungua katika miaka 2 – hadi 5 ya mwanzoni. Kutokana na uchovu wa kipingi cha ujauzito, wasiwasi wa siku ya kujifungua inapokaribia, ukosefu wa usingizi baada ya kujifungua na kubadilika kwa maumbile ya uzazi baada ya kujifungua vinamuathiri sana mwanamke. Mama anaponyesha mtoto upo uwezekana wa kichocheo kiitwacho ESTROGEN kupungua na hivyo kusababisha viungo vya uzazi kuwa na ukavu ambao mwanzoni haukuwepo. Wanawake wanashauriwa kutumia mafuta ya K.Y  Jelly kuondoa ukavu huo.

Kipindi hiki ni kipindi kigumu sana kwa wanaume wasioelewa hali halisi baada ya mwanamke kujifungua. Inashauriwa mwanamke aanze kushiriki ngoma ya wakubwa baada ya wiki sita toka siku aliyojifungua na wanaume wanapashwa kuheshimu hili kuepuka ugomvi au chuki baina yao. Pamoja na hilo ni muhimu kukumbuka kuwa baada ya kujifungua mwanamke hatakuwa na hamu kiasi kile alichokuwa nacho mwanzoni na kwa baadhi ya wanawake inaweza kuchukua mwaka mzima kuweza kurudia kasi ya mwanzoni. Halii hiyo inasababishwa na kichocheo cha PROLACTION ambcho hutoka kwa wingi kwa mama anayenyinyesha. PROLACTIN hupunguza hamu ya mwanamke kucheza ngoma ya wakubwa kwa kupunguza mtiririko wa kichocheo cha hamu kiitwacho ESTROGEN.

Hapa ningependa kutoa angalizo ambalo wengi wanhitaji kulisikia. Mwanamke anapokaribia kujifungua mishipa ya damu iitwayo VEIN katika viungo vya uzazi hupanuka kuliko kawaida yake na hivyo kufanya kuta zake kuwa dhaifu sana. Kuna hatari ya kifo iwapo mwanaume kwa kutumia mdomo wake atachezea maeneo ya viungo vya uzazi vya mwanamke miezi miwili kabla ya kujifungua au miezi miwili kabla ya kujifungua.  Mwanaume akitumia mdomo wake bila kujua anaweza kusababisha hewa kuingia kwenye mishipa hiyo ya vein na kusababisha damu kutofika kwenye ubongo wa mwanamke na kusababisha kifo. Hali hiyo iitwayo AIR EMBOLISM mara nyingi hutokea iwapo mwanamke atashiriki ngoma ya wakubwa kabla ya wiki 6 kuisha.

Jambo linguine la ajabu linalojitokeza pale mama anapojifungua ni kwamba ile hali ya kunyonyesha  mtoto mama anapoteza hamu ya kuguswa na mumewe kwa kuwa tayari anakuwa amepata mguso wa ngozi kwa ngozi toka kwa mtoto na kuona kuguswa na mumewe kama kero ya aina fulani. Wapo wanawake wengine ambao hujisikia raha ya kimahaba pale mtoto anayonyonya chuchu PENZI LINAPOGEKA KUWA KERO

Mahusiano ya kimapenzi ni kitu kizuri sana ndio maana mara ya kwanza mtu anapoingia katika mahusiano ya kimapenzi anakuwa na furaha kubwa sana. Naomba uzingatie kuwa nimesema kuwa mtu anapoingia  katika uhusiano kwa mara ya kwanza, yaani  kama ni mwanaume huyo anakuwa ndie mwanamke wa kwanza kabisa kwake    na   kwa mwanamke huyo ndio  anakuwa mwanaume wa kwanza kabisa. Katika ulimwengu tulionao sasa ni mara  chache sana utaona kuwa mwanaume ambaye hajawahi kuwa na mahusiano ya kimahaba  NA MWANAMKE anaanza na mwanamke ambaye na yeye huyo ndio anaekuwa mwanaume wa kwanza.

Tatizo tulilonalo sasa utakuta mwanaume ambaye tayari ameshakuwa na mahusiano na wanawake 2 anaanza uhusiano na dada ambaye hajakuwa na uhusiano wowote au dada ambaye ameshakuwa na mahusiano na wanaume wawili anaanza mahusiano na mwanaume ambae hajawa katika mahusiano ya kimapenzi.Katika mazingira kama hayo lazima mtu atajikuta analinganisha mpenzi aliene sasa na Yule aliemtangulia.