Thursday, November 13, 2014

HATARI ZA DAWA ZA NGUVU ZA KIUME ZENYE KEMIKALI

Tatizo la nguvu za kiume linalowaathiri mamilioni ya watu na pia kuathiri mahusiano ya kimapenzi .Katika kazi yangu katika Cliniki ya Afya ya Mapenzi asilimia 97% ya wateja wangu ni wanaume na leo nimeona nizungumzie hatari za kutumia madawa mengine yauzwayo katika maduka ya madawa mbalimbali.

Nimeamua kuandika habari hizi baada ya kaka mmoja aliesafiri toka Tabora na kuja kuniona baada ya kwenda katika hospitali ya moja ya rufaa  akiwa na tatizo la kuwahi kumaliza bila kupata msaada. Tatizo hilo limekuwa kero kwa mke wake na hivyo kutaka kuliondoa kwa gharama yeyote ile. Kaka huyo alienda kwa Daktari bingwa wa mambo ya  uume na uke na mambo ya viungo vya uzazi kwa kitaalamu  wanaitwa UROLOGISTS.

Baada ya kuelezea tatizo lake kwa Daktari huyo bingwa alipewa dawa ambazo ni kwa tatizo la nguvu za kiume na hazikumsaidia katika tatizo lake. Nilishangaa kusikia kuwa Daktari bingwa ameshindwa kumsaidia kaka huyo kwani tayari huyo kaka alikuwa anafahamu madhara ya dawa hizo na hivyo kwa kuwa alikuwa tayari amekwisha sikia katika vipindi vyangu vya redio vya USIKU WA MAHABA siku ya Jumatano katika redio FREE AFRIKA alinitafuta alikuja kwangu kama hatua ya mwisho katika mahangaiko yake.Nilifanikiwa kumsaidia na tatizo lake likawa ni historia.

Mwanzoni mwa kazi yangu 2006 nilikuwa nawapa watu dawa hizo zinazouzwa madukani na siku moja Mzee mmoja anaefanya kazi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jijini Mwanza alikuja na malalamiko yanayofanana kabisa na kaka huyo toka Tabora. Nilimweleza juu ya tiba mbili nilizonazo yaani dawa hizo za madukani zinazokupa nguvu ya masaa 4 na dawa yangu ya asili inayoweza kukuondolea tatizo hilo baada ya siku 5 hadi 7.  Baba huyo akachagua dawa hiyo ya haraka akaitumia siku hiyo hiyo ili kumziba mdomo mke wake.

Nilimuuzia dawa hizo baba huyo mwenye umri wa miaka 46 na alienda na kuzitumia hizo dawa. Kesho yake baba huyo alirudi ofisini kwangu na kuniambia kuwa kweli alifanikiwa kumfurahisha mke wake usiku uliopita lakini majira ya saa 9 usiku aliamshwa na maumivu makali ya kichwa na kuiona dunia yote kuwa ni rangi ya njano.
 Nisingependa upate matatizo yanayofanana na hayo na yafuatayo ni uthibitisho wa kisayansi wa madhara ya dawa hizo:-

Kuna tovuti 22 milioni zinazoshabikia madawa mbalimbali ya nguvu za kiume zenye kemikali za hatari kwako  kwa hiyo ni rahisi kushawishiwa na kutapeliwa. Shirika la  kudhibiti madawa na vyakula la huko Marekani limeorodhesha  majina ya madawa yenye madhara kwa mtumiajo na madawa hayo ni Zimayx, vigor – 25, True Man ,Shanghai Ultra, neophase, Nasutra Man up now, Liviro 3 , Libidus, Lady Shanghai, Hs joy of love, Energy Max, Blue steel, Actva Sx ,Activa Rx na Adam free.

Madawa hayo yote na mengineyo yasioorodheshwa hapo hufanya kazi kama ifuatavyo:-
Madawa hayo yana kemikali iitwayo PHOSIPHODIESTERASE 51 (PDE51) na kazi ya PDE51 ni kuzuia nguvu ya Enzyme iitwayo PHOSPHODIESTERASE 5 (PDE5)ambayo ndiyo inayozuia uume kusimama kama inavyotakiwa. Kemikali ya PDE51 inanyonywa ndani ya damu  na ndani ya saa moja mwanaume anakuwa na nguvu ya kumuwezesha kushiriki tendo la ndoa ndani ya masaa yasiozidi 4 kutokana na afya ya mtu mara  nyingi nguvu za dawa hiyo huweza kwenda hadi  masaa 7.

Ubaya wa madawa hayo  na mengine ni kwamba yana kemikali iitwayo GLYBURIDE yenye nguvu ya kuathiri mapigo ya moyo na kushusha presha ya damu ambayo ni hatari sana. Mwaka 2008 huko mjini Singapore watu 150 walilazwa hospitalini kutokana na kutumia madawa hayo.

Shirika la kuthibiti madawa la Marekani la FDA lilifanya upelelezi na kugundua kuwa madawa mengi ya nguvu za kiume yana kemikali ambazo ni za hatari.

Dalili za kuwa umeanza kuathirika na madawa hayo  UNAPOZITUMIA ni hizi zifuatazo:-

(1)        Maumivu ya misuli.
(2)        Kupata shida ya upumuaji.
(3)        Maumivu ya kichwa.
(4)        Maumivu ya macho au kulegea kwa macho.
(5)        Kupiga chafya ovyo ovyo.
(6)        Kuvurugika kwa tumbo mara baada ya kula chakula.
(7)        Mafua.
(8)        Kupata shida kupata usingizi.
(9)        Ngozi kuwa na joto lisilo la kawaida.
(10)     Maumivu ya masikio.
(11)     Kichefuchefu.
(12)     Ulimi kuwa mwekundu kuliko kawaida.
(13)     Kushindwa kumwaga mbegu hata ukifanya tendo la ndoa kwa muda mrefu.
(14)     Kuona dunia imebadilika rangi.
(15)     Kuwa na hali ya wasiwasi bila ya sababu yeyote.
(16)     Maumivu kifuani.
(17)     Kutokuona sawa sawa.
(18)     Njaa ya kupita kiasi.
(19)     Kuongezeka kwa ukubwa wa mboni ya jicho.
(20)     Kutokwa jasho sana.
(21)     Maumivu ya mgongo.
(22)     Kutopendelea mwanga mkali.
(23)     Uchovu wa bila sababu.


Ndugu nimeandika hayo kufumbua macho uone kwa yapo madhara na ukitaka uhakika iwapo unafahamu kiingereza tafuta kwenye GOOGLE kwa kuandika ED drugs are harmful na utajionea mwenyewe ukweli huo.


Dawa ya PRIKA utakayoiona katika blog hii ni ya asilia kwani imetokana na mimea halisi na haifanyi kazi mpaka imetanguliwa na mazoezi maalumu utakayofanya ukiwa umekaa kwenye kiti. Uanzapo kutumia dawa hii ya PRIKA utaanza kuona mabadiliko baada ya siku 5 – 7 lakini utaitumia dawa hiyo kwa wiki mbili ili kulifuta tatizo la nguvu za kiume na la kuwahi kumaliza .Unapoagiza dawa hiyo utapewa kijarida kitakachokupa maelekezo ya kutumia dawa hiyo na pia maelekezo ya mambo ya kuepuka ili tatizo hilo lisikurudie tena maisha yako yote.

Sunday, November 2, 2014

Tamaa Tamu


TAMAA TAMU

Ni kweli tendo la ndoa ni tamu kivyakevyake na huwezi kulinganisha na kitu kingine chochote lakini tunapaswa kuangalia jinsi tamaa ya utamu huo ilivyo na jinsi ya kuitumia kujenga penzi linalotosheleza. Asilimia kubwa ya wanaume wanaonekana kama vile hawawezi kutosheka kuwa na mwanamke mmoja na pia wapo baadhi ya wanawake ambao nao wanaona kuwa hawawezi kutosheka na mwanaume mmoja.

Wataalamu wa sayansi ya mapenzi wamegundua kuwa kila mtu anahitaji mambo fulani ili aweze kujisikia kuwa ametosheka na tendo la ndoa na hali hiyo inaitwa kwa kiingereza FETISH. FETISH ni jambo ambalo unaliona kuwa bila ya kuwepo kwa jambo hilo huwezi kutosheka na tendo la ndoa na kwa bahati mbaya watu wengi hawajui kuwa wanao udhaifu wa aina hii,udhaifu wa ajabu sana.

Neno FETISH limetokana na lugha ya Kireno FETICO,neno hilo hutumika  ikimaanisha nguvu ya kichawi. Kila mmoja anao udhaifu wa aina hii japo hatufahamu jinsi nguvu yake inavyotuendesha katika mahusiano yetu ya kimapenzi. Hali ya mtu kupenda mwanamke mwenye hipsi na makalio ya aina fulani hiyo iko katika kundi la  fethish, mwanamke kupenda mwanaume mrefu mwenye misuli ,mwanaume mwenye sauti nzito na hiyo ni fetishi yake.Mwanamke anayependelea mwanaume mwenue kifua kilicojaanywele kwa mfano atapata shida kuridhika iwapo mumewe hana nywele hizo.Mfano huo unaweza kuupeleka kwa ukubwa wa uume pia.

Kuna aina nyingi za MAFETISHI na nyingine ni za ajabu sana lakini ambazo zimetawala kwa watu wengi ni hizi zifuatazo:-

(1)       VOYEURISM 
Hii ni tamaa inayojitokeza pale uonapo maumbile ya mwili wa mtu wa tofauti na jinsia yako. Tamaa hii inachochewa na nguvu na uvaaji wa nguo zinazobana au zinazoacha wazi maeneo fulani ya mwili.

(2)       PYGOPHILIA
Hii ni tamaa ya kutamani mtu mwenye makalio ya muundo fulani au kujikuta unapata msisimko mkali uonapo mtu mwenye makalio ya aina hiyo tamaa hii inawasumbua zaidi wanaume ambao wanataka wanawake wote wawe na makalio kama ya Jenifer Lopez (JLO).Utafiti uliofanyika na mashirika ya bima huko uingereza umeonyesha kuwa wanaume wengi husababisha ajali za magari hasa wakati wa kiangazi ambapo wanawake wengi huvaa nguo fupi na zenye kubana na kuonyesha uzuri wa makalio.

(3)       RETIFISM
Hii ni tamaa inayoamshwa pale uonapo mwanamke aliyevaa viatu virefu (mchuchumio).
(4)       TRICHOPHILIA
Hii ni tamaa ambayo hujitokeza kwa mtu akutanapo na mtu mwenye aina fulani ya nywele au wigi fulani la nywele. Hii inaweza kuwa hata nywele za kifuani.

(5)       DOMINATION AND SUBMISSION
Hii tamaa  imewabana watu wengi  na hawajui kuwa inawatawala na hivyo kushindwa kujua jinsi ya kukabiliana nayo ili kuongezea penzi kati yao. Mara nyingi wakati wa tendo la ndoa mwanaume huwa juu na mwanamke huwa chini na wengi huona kuwa ni hali ya kawaida kabisa lakini kwa kutokujua nguvu ya desturi hiyo wengi wamewazoesha wapenzi wao.Mindo huo utumikapo mara kwa mara unamfanya mwanaume ajione zaidi kuwa yeye ndiye mbabe na hahitaji ushauriau msaada toka kwa mkewe. Kwa mpenzi ambaye yeye anapata raha zaidi kwa kumfanyia mambo fulani fulani mpenzi wake ni muhimu apewe nafasi hiyo  ili ajione kuwa ni wa muhimu na mwenye nguvu. Hivyo basi iwapo mpenzi wako atakuwa mwenye haraka au asiependelea tendo la ndoa lichukue zaidi ya nusu saa huyo atakuwa anajiharibia uhusiano wake mwenyewe bila kujua. Watu wengi huchanganyikiwa hapa kwani kuna wengine ambao wanapenda kutoa starehe kwa wapenzi wao wakiwa wametulia  jambo ambalo humfanya mpenzi aboreke. Wengine hupendelea kubadilishana nafasi kwa kupokezana  mmoja amwandae mwenziwe na baadae na wao wanataka watulie na kumwachia mpenzi kazi ya kumletea utamu wa tendo la ndoa DOMINATION NA SUBMISSION kwa Kiswahili ni KUTAWALA  NA KUTAWALIWA (au kwa maneno mengine ni kama kukandamiza na kukandamizwa). Ni muhimu kwa wapendanao kutambua umuhimu wa mtindo huu kwani una nguvu kubwa sana ukitumiwa vizuri katika kipindi cha tendo la ndoa. Katika utafiti wangu juu ya kuongezea utamu wa tendo la ndoa nilifikia hatua ya kuanza kuangalia jinsi wasagaji, yaani wanawake wanaofanya mapenzi na wanawake wenzao na huko niliona nguvu ya mtindo huo. Baada ya kuangalia kwa muda fulani nilielewa kwanini mwanamke ambaye ameingia kwenye usagaji atapata shida kubwa kufurahia tendo la ndoa na mwanaume na wengi hufikia hatua ya kuwachukia wanaume.

Changamoto kwa wapendanao ni kwamba upo umuhimu wa kutumia mtindo huu wa KUTAWALA NA KUTAWALIWA katika kuboresha utamu wa tendo la ndoa na kuondosha hali ya mpenzi kuboreka na mpenzi wake wa muda mrefu. Ili uweze kufanikiwa katika hili ni muhimu upige vita woga na aibu. Nakutakia heri katika kutengeneza utamu zaidi wa tamaa ya tendo la ndoa.