Sunday, November 2, 2014

Tamaa Tamu


TAMAA TAMU

Ni kweli tendo la ndoa ni tamu kivyakevyake na huwezi kulinganisha na kitu kingine chochote lakini tunapaswa kuangalia jinsi tamaa ya utamu huo ilivyo na jinsi ya kuitumia kujenga penzi linalotosheleza. Asilimia kubwa ya wanaume wanaonekana kama vile hawawezi kutosheka kuwa na mwanamke mmoja na pia wapo baadhi ya wanawake ambao nao wanaona kuwa hawawezi kutosheka na mwanaume mmoja.

Wataalamu wa sayansi ya mapenzi wamegundua kuwa kila mtu anahitaji mambo fulani ili aweze kujisikia kuwa ametosheka na tendo la ndoa na hali hiyo inaitwa kwa kiingereza FETISH. FETISH ni jambo ambalo unaliona kuwa bila ya kuwepo kwa jambo hilo huwezi kutosheka na tendo la ndoa na kwa bahati mbaya watu wengi hawajui kuwa wanao udhaifu wa aina hii,udhaifu wa ajabu sana.

Neno FETISH limetokana na lugha ya Kireno FETICO,neno hilo hutumika  ikimaanisha nguvu ya kichawi. Kila mmoja anao udhaifu wa aina hii japo hatufahamu jinsi nguvu yake inavyotuendesha katika mahusiano yetu ya kimapenzi. Hali ya mtu kupenda mwanamke mwenye hipsi na makalio ya aina fulani hiyo iko katika kundi la  fethish, mwanamke kupenda mwanaume mrefu mwenye misuli ,mwanaume mwenye sauti nzito na hiyo ni fetishi yake.Mwanamke anayependelea mwanaume mwenue kifua kilicojaanywele kwa mfano atapata shida kuridhika iwapo mumewe hana nywele hizo.Mfano huo unaweza kuupeleka kwa ukubwa wa uume pia.

Kuna aina nyingi za MAFETISHI na nyingine ni za ajabu sana lakini ambazo zimetawala kwa watu wengi ni hizi zifuatazo:-

(1)       VOYEURISM 
Hii ni tamaa inayojitokeza pale uonapo maumbile ya mwili wa mtu wa tofauti na jinsia yako. Tamaa hii inachochewa na nguvu na uvaaji wa nguo zinazobana au zinazoacha wazi maeneo fulani ya mwili.

(2)       PYGOPHILIA
Hii ni tamaa ya kutamani mtu mwenye makalio ya muundo fulani au kujikuta unapata msisimko mkali uonapo mtu mwenye makalio ya aina hiyo tamaa hii inawasumbua zaidi wanaume ambao wanataka wanawake wote wawe na makalio kama ya Jenifer Lopez (JLO).Utafiti uliofanyika na mashirika ya bima huko uingereza umeonyesha kuwa wanaume wengi husababisha ajali za magari hasa wakati wa kiangazi ambapo wanawake wengi huvaa nguo fupi na zenye kubana na kuonyesha uzuri wa makalio.

(3)       RETIFISM
Hii ni tamaa inayoamshwa pale uonapo mwanamke aliyevaa viatu virefu (mchuchumio).
(4)       TRICHOPHILIA
Hii ni tamaa ambayo hujitokeza kwa mtu akutanapo na mtu mwenye aina fulani ya nywele au wigi fulani la nywele. Hii inaweza kuwa hata nywele za kifuani.

(5)       DOMINATION AND SUBMISSION
Hii tamaa  imewabana watu wengi  na hawajui kuwa inawatawala na hivyo kushindwa kujua jinsi ya kukabiliana nayo ili kuongezea penzi kati yao. Mara nyingi wakati wa tendo la ndoa mwanaume huwa juu na mwanamke huwa chini na wengi huona kuwa ni hali ya kawaida kabisa lakini kwa kutokujua nguvu ya desturi hiyo wengi wamewazoesha wapenzi wao.Mindo huo utumikapo mara kwa mara unamfanya mwanaume ajione zaidi kuwa yeye ndiye mbabe na hahitaji ushauriau msaada toka kwa mkewe. Kwa mpenzi ambaye yeye anapata raha zaidi kwa kumfanyia mambo fulani fulani mpenzi wake ni muhimu apewe nafasi hiyo  ili ajione kuwa ni wa muhimu na mwenye nguvu. Hivyo basi iwapo mpenzi wako atakuwa mwenye haraka au asiependelea tendo la ndoa lichukue zaidi ya nusu saa huyo atakuwa anajiharibia uhusiano wake mwenyewe bila kujua. Watu wengi huchanganyikiwa hapa kwani kuna wengine ambao wanapenda kutoa starehe kwa wapenzi wao wakiwa wametulia  jambo ambalo humfanya mpenzi aboreke. Wengine hupendelea kubadilishana nafasi kwa kupokezana  mmoja amwandae mwenziwe na baadae na wao wanataka watulie na kumwachia mpenzi kazi ya kumletea utamu wa tendo la ndoa DOMINATION NA SUBMISSION kwa Kiswahili ni KUTAWALA  NA KUTAWALIWA (au kwa maneno mengine ni kama kukandamiza na kukandamizwa). Ni muhimu kwa wapendanao kutambua umuhimu wa mtindo huu kwani una nguvu kubwa sana ukitumiwa vizuri katika kipindi cha tendo la ndoa. Katika utafiti wangu juu ya kuongezea utamu wa tendo la ndoa nilifikia hatua ya kuanza kuangalia jinsi wasagaji, yaani wanawake wanaofanya mapenzi na wanawake wenzao na huko niliona nguvu ya mtindo huo. Baada ya kuangalia kwa muda fulani nilielewa kwanini mwanamke ambaye ameingia kwenye usagaji atapata shida kubwa kufurahia tendo la ndoa na mwanaume na wengi hufikia hatua ya kuwachukia wanaume.

Changamoto kwa wapendanao ni kwamba upo umuhimu wa kutumia mtindo huu wa KUTAWALA NA KUTAWALIWA katika kuboresha utamu wa tendo la ndoa na kuondosha hali ya mpenzi kuboreka na mpenzi wake wa muda mrefu. Ili uweze kufanikiwa katika hili ni muhimu upige vita woga na aibu. Nakutakia heri katika kutengeneza utamu zaidi wa tamaa ya tendo la ndoa.   

1 comment: